18 Mei 2021 - 10:52
Amnesty International yalaani mashambulio ya kikatili ya Israel dhidi ya Wapalestina

Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, limelaani vikali jinai zinazotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na kusema kuwa jinai hizo ni sawa na jinai za kivita.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika hilo limesema kwamba Israel inalenga moja kwa moja nyumba na makazi ya raia na hivyo kutowapa fursa ya kukimbia na kuokoa maisha yao.

Katika mashambulio ya kinyama yanayotekelezwa na utawala wa kigaidi wa Israel katika Ukanda wa Gaza tokea Jumatatu wiki iliyopita, zaidi ya Wapalestina 220 wakiwemo watoto 60 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 5600 kujeruhiwa.

Katika moja ya mashambulio ya kinyama ambayo yametekelezwa leo afajiri na utawala wa Israel dhidi ya makazi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, majumba mawili yamelengwa na kubomolewa kabisa ambapo watu wapatao 30 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa kinyama katika hujuma hiyo.

Yussuf Yassin ambaye ni mmoja wa timu ya madaktari katika ukanda huo amewaambia wachunguzi wa shirika la Amnesty International kwamba shambulio hilo la kinyama limefanywa bila kutolewa onyo lolote na ndio maana wakazi wa majengo hayo hawakuona haya ya kuyahama.

Utawala haramu wa Israel unafanya mashambulio ya kijinai katika Ukanda wa Gaza tokea tarehe 10 mwezi huu ambapo unashambulia kiholela makazi ya raia kwa ndege za kivita na mabomu na hivyo kuua kinyama raia wa kawaida na hasa wanawake na watoto wadogo wasio na hatia.

Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya vikao vya dharura mara tatu kwa ajili ya kujaribu kusimamisha mashambulio hayo ya Israel katika Ukanda wa Gaza lakini bila mafanikio yoyoye, na hilo ni kutokana na ukwamishaji wa Marekani ambayo haitaki utawala huo uchukuliwe hatua za kisheria.

342/